Friday, October 28, 2011

MASHUJAA WA TAIFA

     Kwa kila nchi kuna Mashujaa ambao wamesababisha uhuru kupatikana kwa namna moja ama nyingine.Iwe kwa kumwaga damu ama kutokumwaga damu.Katika nchi yetu kuna mashujaa waliofanikisha kutuletea uhuru wetu hivyo basi inapaswa kutambua kazi zao kwa Taifa na sio mpaka kipindi cha uhuru kina karibia ndio tunawakumbuka kwa wema wao walio fanya zidi ya Taifa letu.
     Inatupaswa kuwajenge mazingira mazuri ya kujiona kweli ni mashuujaa wa taifa na kujenga msingi imara zidi ya vizazi vijavyo kutambua wana harakati wa taifa hili.na kuonyesha ni jinsi gani walipigania taifa ili iwe somo zuri kwao na kufata nyendo zao katika kujenga taifa lililo bora na sio kusifia mashuujaa wa nchi za ng'ambo.
                      TAIFA IMARA HUJENGWA NA WANANCHI WENYEWE.

Monday, October 24, 2011

MAFANIKIO HULETWA NA MWENYEWE KWA JUHUDI ZAKO.

      Katika maisha kuna mambo mengi sana hutokea yaweza kuwa mazuri  au mabaya.Pia kuna kufanikiwa na kutokufanikiwa katika maisha yanayo tuzunguka kwa namna moja ama nyingine.Na mafaniko mazuri hayaji kwa kuyangojea bali kuyafata huko yaliko.                                                                                                    
       Hivyo basi juhudi na uwezo wa kufanya kazi ndio njia sahihi ya kufanikiwa katika maisha na si kungojea mafanikio yakufate hapo uliko utakua una poteza muda na miaka inazidi kwenda.Pia mawazo mazuri ya watu huleta hamasa katika mafanikio yako uwe unasoma au mfanyakazi bila mawazo ya watu huwezi kuendelea mbele katika mambo yako.
        Pia ukiwa na wivu wa maendeleo uongeza hamasa katika shughuli zako penda kujifunza mambo mengi na hata kama utaiga yale unayo yaona yanakufaa katika kazi zako za kila siku,kwani maendeloo huletwa na mwenyewe na sio mtu mwingine.NGUVU,JUHUDI NA KUJITUMA huleta mafanikio yalio bora.

Monday, October 17, 2011